Kila jambo maishani lina kanuni zake. Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushirikiana na Mungu.
|
Kanuni Ya |
|
MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO. |
UPENDO WA MUNGU
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16
MPANGO WA MUNGU KWAKO
Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10
Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo?
Ni kwa sababu . . .
|
Kanuni Ya |
|
MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na Mungu. Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake. |
| MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI |
| Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. | Warumi 3:23 |
Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.
| MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU |
| Lakini maovu yenu imewatenga ninyi na Mungu wenu. | Isaya 59:2 |
![]() |
MunguMtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi. |
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .
|
Kanuni Ya |
|
YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu. |
| ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU |
| Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu. | 1 Petro 3:18 |
| YESU YUHAI |
| Kristo alikufa kwa ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko. | 1 Wakorintho 15:3,4 |
| YESU NDIYE NJIA YA PEKEE |
| Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. | Yohana 14:6 |
![]() | Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu. |
Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .
|
Kanuni Ya |
|
INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako. |
| UNAMPOKEAKRISTO KWA IMANI |
| Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. | Yohana 1:12 |
| Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. | Waefeso 2:8,9 |
| INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO |
| Tazama, nasimama miangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . . |
Kumpokea Yesu Kristo ni:

Je, ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano wa maisha yako?
Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?
UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.
| Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin. |
Je, sala hii ni sawa na haja ya mayo wako?
Kama sala hii ni sawa haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.
JINSI YA KWAMBA YESU YUMO MAISHANI MWAKO
Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.
| ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE |
| Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu. | 1 Yohana 5:11-13 |
Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.
USIYATEGEMEE MAWAZO YA MOYO WAKO.
Unaweza kujisikia leo unafuraha ndipo kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. Waebrania 13:5.

Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.
Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.
KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.
Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?
Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imaniyetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.
Tuombe tukiwa huru.
Na sasa je?
JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:
NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA
Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)
Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikilundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.
Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.
Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.
|
ADDITIONAL ASSISTANCE If you've just asked Jesus Christ into your life, please click here and tell us about it. We would love to hear from you and help you grow in your faith. If you still have a question, please click here. |
| © 1995-2001 Campus Crusade for Christ International Questions and Comments are always welcome! http://www.4laws.com/laws/swahili/default.htm |